
Yanga ni club ya mashabiki
mbalimbali wenye itikadi tofauti, sasa sio sawa kuweka mabango ya
kisiasa kwenye ofisi za club. Sina uhakika kama viongozi wa club hii
wameliona hili lakini kwanini wasione wakati lipo nje ya ofisi yao.
Yanga kama club ya wananchi ina
jukumu la kutetea demokrasia na wasioneshe hata chembe moja kwa moja
kuhusisha club na chama chochote cha siasa.
Natoa rai karatasi hii itolewe na
hata vilabu vingine au asasi zozote za kijamii zisijihusishe moja kwa
moja na vyama vya siasa. Mtu binafsi anaweza kujihusisha lakini sio
club. +255 kwanza kabla ya kitu chochote
No comments:
Post a Comment