Jaja Ndio Tatizo kwa Kusainiwa Mkataba a Emerson
BAADA ya kutua nchini jana akitokea kwao Brazil, kiungo mkabaji Emerson
de Oliveira Neves Roque ameanza mazoezi mepesi akiwa na Kikosi cha Yanga
kwenye uwanja wa shule ya sekondari Loyola jijini Dar es Salaam leo
huku uongozi wa Yanga ukisita kumpa mkataba.Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu amesema jijini Dar es Salaam leo kuwa
haijulikani lini kiungo huyo atapewa mkataba wa kuitumikia klabu hiyo ya
Jangwani.
“Siwezi kutabiri Emerson atapewa mkataba lini,” amejibu kwa kifupi Njovu
baada ya kuulizwa na mtandao huu huku kukiwa na taarifa kwamba uongozi
wa Yanga hautaki kukurupuka kumpa mkataba mchezaji huyo hadi pale
atakapofuzu majaribio na vipimo vya afya kwa kuwa kocha mkuu Mbrazil
Marcio Maximo aliuingiza mkenge kwa mshambuliaji aliyetimka Genilson
Santos Santana ‘Jaja’.Jaja aliyeifungia Yanga mabao sita katika mechi 11 (moja katika mechi
saba za Ligi Kuu ya Vodacopm Tanzania Bara – VPL) alizocheza katika
kikosi cha Maximo, amedaiwa na uongozi wa klabu hiyo ya Jangwani kukataa
kurejea nchini baada ya mapumziko kutokana na kinachodaiwa kukumbwa na
matatizo ya kifamilia.Pengine, uongozi wa wanajangwani umeamua kumalizana naye kistaarabu baada ya kutoridhishwa na kiwango chake.Mshambuliaji huyo aliyekuwa ameteka vichwa vya vyombo vya habari nchini
wakati wa ujio wake uliokwenda sanjari na kiungo Mbrazil mwenzake Andrey
Coutinho ameshindwa kung’ara VPL licha ya kufunga magoli mawili ya
video katika mechi ya Ngao ya Jamii waliyoinyanyasa Azam FC kwa kuipa
kipigo cha mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Septemba 14.Emerson aliyesafiri kwa zaidi ya saa 11 kutoka jijini Rio de Janeiro,
Brazil, ameungana na wachezaji wengine wa Yanga katika mazoezi ya leo
ambayo yalikuwa ya kukimbia kimbia yaliyofanyika chini ya Maximo na
msaidizi Leonardo Neiva raia wa Brazil pia.Waandishi wa habari na mashabiki wa Yanga hawakuruhusiwa kuingia kwenye
uwanja huo leo na wamelazimika kuyafuatilia mazoezi hayo wakiwa nje ya
uzio unaozunguka uwanja na shule hiyo.Endapo Emerson akifuzu majaribio na vipimo vya afya, imeelezwa na
uongozi wa Yanga kwamba ataingia mkataba na klabu hiyo ili aitumikie VPL
na michuano ya kimataifa. Yanga itakuwa mwakilishi wa Tanzania Bara
katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Africa
No comments:
Post a Comment