Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Saturday, September 20, 2014

Mgambo waandika Historia Mkwakwani stadium

Kocha wa Mgambo baada ya Mechi       




Ligi kuu ya soka Tanzania Bara imeanza
 Leo katika viwanja mbambali nchini huku
ikishuhudia matokeo ya aina yake
yakipatikana.Katika uwanja wa Mkwakwani
mjini Tanga Timu ya Mgambo Shooting ya
Kabuku-Handeni Tanga imeanza kwa
Kishindo katika historia yake ya miaka mitatu
ya ushiriki wa ligi kuu Tanzania Bara kwa
kuibamiza timu ya Kagera Sugar bao moja
kwa sifuri bao lililowekwa kimiani na PERA
Ramadhani katika dakika ya sita ya mchezo,
Mchezo huo uliojaa ufundi mwingi hasa kwa
 Upande wa Mgambo ambao walionekana
kucheza soka la kitabuni muda wote wa
mchezo huo,Ikumbukwe Mgambo shooting
haijawahi kushinda mechi ya kwanza katika
historia ya ligi kuu na Msimu uliopita walipata
points sita raundi ya kwanza ya ligi hivyo kwa
matokeo haya inaonyesha Mwaka huu
watafanya maajabu makubwa katika ligi..

Katika mchezo mwengine kule katika
mji kasoro bahari Morogoro Timu ya
Mtibwa sugar Imeibamiza bila huruma
timu ya Yanga sports club kwa mabao
mawili bila majibu na kuwaacha wakongwe
hao wa soka Tanzania hoi bin taabani na
ikishuhudia Nyota wake kutoka Brazil akikosa
Penalt.Mtibwa ina historia ya kuichachafya
Yanga kila Msimu hivyo kuendeleza record
 yake waliyojiwekea,
Kwingineko Timu zilizopanda daraja
zilionyeshana kazi pale mjini Shinyanga kwa
timu ya Ndanda F.C Kuibamiza timu ya
Stand United kwa mabao Manne kwa Bila
 katika  mchezo ulioshuhudia Ndanda Ikiongoza
ligi katika mzunguko huu wa kwanza ukisubiria
mchezo mmoja tu baina ya Simba na Wagosi
wa Kaya hapo kesho katika uwanja wa Taifa
na ikumbukwe mechi iliyopita Wagosi
waliwafunga Simba Sports katika Uwanja
huo bao moja kwa sifuri,Matokea mengine ni
AZAM 3-POLISI 1
RUVU SHOOTING 0-PRISON 2

No comments:

Post a Comment