Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Saturday, February 21, 2015

Mgambo Watakata Wagosi Hoi Mtwara

Timu ya soka ya Mgambo shooting ya Tanga leo
imewafundisha mpira wakata Miwa wa Mtibwa
kwa kuwafunga goli moja kwa sifuri katika mchezo
mzuri na wa kusisimua uliopigwa katika uwanja wa
mkwakwani.Katika pambano hilo Mchezaji Malimi
busungu aliibuka kuwa shujaa wa Mgambo kwa
kuwachachafyya Mtibwa katika muda wote wa Mchezo.
Alifanikiwa kufunga magoli mawili lakini mwamuzi wa
pembeni alikataa moja jambo lililoamsha taharuki kwa
mashabiki walioingia uwanjani hapo.kwa matokeo
hayo Mgambo anafikisha alama 17 na anatarajiwa kukutana
na timu ya Coastal Union,
kule ndanda timu ya Coastal union ya hapa imechapwa
na Ndanda kwa ushindi mwembamba wa goli moja kwa
sifuri.

No comments:

Post a Comment