wakazi wa Tanga na vitongoji vyake kwa kuwabamiza bila
huruma timu ya Majimaji ya Songea kwa Ushindi wa goli
moja kwa bila.
Ilikuwa ni katika kipindi cha kwanza wakati Mgambo
ilipojipatia bao baada ya Krosi ya kutoka kwa Cholo
kuenda moja kwa moja Kichwani kwa Kapteni wa
Mgambo Fulmence Maganga na Kuutia Kimiani huku
kipa wa Majimaji akitapatapa bila ya msaada wowote.
Kwa ushindi huo Mgambo JKT Inajikusanyia alama
4 baada ya michezo mitatu hivyo kuwapa matumaini
wakazi wa Tanga.
Leo katika uwanja huo huo wa Mkwakwani Wagosi
wa kaya Coastal Union Watapepetana na Toto Africa
ya Mwanza katika Mchezo ambao wakazi wa Tanga
wanataka kuiona Timu yao kwa mara ya kwanza baada
ya kuwa nje ya kituo kwa Mechi mbili na kutokuambulia
alama yoyote.
No comments:
Post a Comment