Timu ya Soka ya Mbeya City inazidi kujidhihirishia kuwa wanaabudu na kuamini sana mambo ya Kishirikina baada ya wiki iliyopita katika Uwanja wa Mkwakwani kuingiza mashabiki siku moja kabla ya Mechi badala ya timu sasa wametoa mpya kule katika uwanja wao wa Nyumbani Sokoine
Katika kile kinachoonekana kuwa na imani za kishirikina, watu
wanaodhaniwa kuwa ni Mbeya City juzi mara baada ya mchezo kati ya Yanga na Prisons
kumalizika, waliingia kwenye Uwanja wa Sokoine uliopo mjini hapa kwa ajili ya
kufanya lindo ili ‘usiharibiwe’.
Watu hao walionekana kutokuwa na imani na kila mtu aliyekuwa
akikatiza katika nyasi za uwanja huo, ambapo walionyesha ukali kwa kila
aliyekiuka na hali kama hiyo ilimkuta pia shabiki maarufu wa Yanga anayetumia
staili ya kujipaka masizi usoni na kujaza nguo nyingi tumboni, maarufu kama
Ally Yanga.
Shuhuda wetu, alishuhudia watu hao mara baada ya mahojiano ya makocha wa Prisons na Yanga wakikataza kupitia hata kando ya uwanja huo kwa kudai kuwa kuna watu wanataka kufanya uchawi.
“Tupo kwa ajili ya kuhakikisha kuwa uwanja hauharibiwi kwa
chochote, iwe imani za kishirikina au kwa njia nyingine, wenzetu wamefungwa
hapa na hatutaki na sisi kupoteza mchezo,” alisema mtu huyo aliyekataa kutaja
jina lake.
Katika hatua nyingine, kikosi cha Mbeya City kilikuwa mafichoni tangu Yanga ilipowasili Jumatatu katika jiji hilo na kujifua kulinda heshima ya nyumbani.
Yanga haijawahi kuifunga Mbeya City katika Uwanja wa Sokoine tangu ilipopanda ligi kuu msimu uliopita na kesho wanakutana kwa mara ya pili kwenye uwanja huo.

No comments:
Post a Comment