Kocha wa Manchester United Luis Van Gaal ameitaka
timu yake ya Manchester united kuendeleza wimbi la
Ushindi katika Kombe la chama cha soka nchini humo
F.A,Maneno hayo ameyasema baada ya kuishuhudia timu
yake ikishinda kwa ushindi wa bao tatu kwa bila dhidi ya
timu ya madaraja ya chini ya Cambridge United.Katika
mchezo huo ambao ulikuwa wa marudio baada ya mchezo
wa kwanza uliopigwa katika uwanja wa Cambrige
kutofungana.Magoli ya United yalifungwa na Juan Mata,
Marcos Rojo na James Wilson yalitosha kabisa kuipitisha
Man United katika hatua nyengine ya michuano hiyo.Kocha
huyo amejigamba na kusema kuwa mara zote anapoingia
kwenye klabu kwa mara ya kwanzalazima nipate kombe
na hapa katika kombe hili sisi ndio timu iliyopita kwa
kishindo na timu kubwa iliyobaki,Mimi sio mtu wa Casino
ila nafikiri sisi tuna nafasi kubwa sana ya kuchukua Kombe
hili kwa sasa,Manchester united haijawahi kuchukua kombe
hilo kwa kipindi cha miaka kumi na moja,Kwa makocha,
wafanyakazi,na wapenzi wetu wote tunataka kushinda
kombe hili.United ilikoswa koswa mapema na Elliot kwa
shuti lililopiga mwamba na Van Gaal alisema ilikuwa ni
bahati kwetu kwani wangepata goli hali yetu ingekuwa
ngumu.Nilimtoa Van Persie kwa ajili ya kumuandaa na
mechi inayokuja na Westham United,Shukrani hatukuruhusu
bao lolote.
No comments:
Post a Comment