Ligi kuu ya soka ya England almaarufu Premier league imeendelea wiki hii baada ya timu vigogo za ligi hiyo Arsenal na Manchester united kutoa Vipigo viwili vitakatifu kwa wapinzani wao,Manchester united ndio walioanza jana kwa kuwabamiza bila huruma Leicester City kwa mabao matatu kwa moja katika Mchezo uuliochezwa katika uwanja wa Old Trafford,Timu hizo katika Round ya kwanza manchester united ilichapwa kwa mabao 5 kwa 1 hivyo kwa mechi ya jana imekuwa kama kulipa kisasi kwa manchester united,magoli ya Man United yamefungwa na Van Persie,Falcao na Wilson,wakati magoli ya Arsenal yamefungwa na Ozil,Giroud,Carzola na Theo Walcot kwa matokeo hayo Arsenal inapata alama 42 huku Manchester wakiwa na Alama 43 |
|
|
|
|
|
No comments:
Post a Comment