Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Sunday, January 18, 2015

Van Gaal Asisitiza kuendelea na Mfumo wa Diamond na Sio 4-4-2

Luis Van Gaal
Kocha mkuu wa Manchester United Luis Van Gaal amesisitiza
kuendelea na mfumo wa almasi badala ya ule wa 4-4-2 ambao
mashabiki walikuwa wakiimba kila mara kutokea jukwaani ktk
pambano lao la jana dhidi ya QPR.Mashabiki hao walisikika
wakiimba 4-4-2.4-4-2 na katika kipindi cha pili kocha huyo
alisikia kilioa chao na kukubali kubadilisha mfumo huo na ukazaa
matunda kwa Manchester kupata ushindi wa mabao mawili kwa
bila.Nafahamu fika tunapocheza na Viungo wanne katikati inakuwa
rahisi kutengeneza nafasi lakini uwiano wa timu unakuwa mbaya
sana,hatari golini kwetu zinakuwa nyingi sana.Tutacheza mpira
kulingana na timu tunayokutana nayo,kama jana tulicheza watakavyo
QPR Katika kipindi cha kwanza,mipira mirefu na mashambulizi ya
kushtukiza lakini kipindi cha pili tulibadilika na ndio tukapata mabao.
Kuhusiana na Radamel Falcao..kwa nianavyo mimi amecheza
vizuri sana japo yeye mwenyewe hakuwa na furaha kwa sababu
hakufunga goli,hiyo ni kawaida kwa washambuliaji wote duniani.

No comments:

Post a Comment