Timu ya Soka Ya Mgambo Shooting Ya Handeni
Kabuku Tanga Leo kwa Mara ya Kwanza imepata\
Sare ya Bila Kufungana Dhidi ya Prison ya Mbeya
katika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.mchezo
huo wa kumi katika mzunguko wa Ligi kuu ya soka
Tanzania bara Vodacom,Katika Mchezo huo timu ya
Prison ilikuwa inajihami kwa muda wote wa mchezo
huku Mgambo ikiwa inafanya mashambulizi ya hapa
na pale.Kwa matokeo hayo Prison inaendelea kuwa
chini ya Msimamo wa ligi huku Mgambo ikijisogeza
juu kwa kukamata Point 13 katika Michezo hiyo 10.
Kesho katika uwanja huu huu wa Mkwakwani Tanga
wagosi wa Kaya Coastal Union watajitupa Uwanjani
kwa kupepetana na Polisi Moro.

No comments:
Post a Comment