Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Monday, January 26, 2015

Safari ya Matumaini ya Wanakimanu manu leo Inaingia PATAMU

Timu ya soka ya African Sports ya Tanga almaarufu wana Kimanumanu
leo ina Mtihani Mgumu dhidi ya timu waliyopambana nayo kwa muda mrefu
kileleni mwa msimamo wa ligi soka daraja la kwanza ya MAJIMAJI songea,
Timu hizo zilikuwa zikuchuana kwa muda mrefu katika ligi hiyo ambapo ni
juzi tu African sports ndio walichukua kijiti cha uongozi wa ligi kwa timu ya
 majimaji ya Songea Kileleni mwa msimamo.Mchezo huo kama wana kimanu
manu wakishinda wanaweza kupanda daraja kuingia Ligi kuu kama watashinda
mechi moja tu iliyobakia hapa Nyumbani kwani baada ya hapo watatoka
kwenda Iringa halafu Dar-es-salaam dhidi ya Friends Rangers.Kwa sasa Jijini
Tanga Mashabiki wa soka wamekaa mkao wa kula kuisubiria Wana kimanu
manu baada ya miaka 25 ya kuwa Nje ya Ligi ya Juu kabisa Nchini.
Bendera za timu hiyo zinashuhudiwa zikipepea kwa Takribani majuma matatu
sasa huku watu wakipokezana kuzilinda na kuziweka Vizuri mara kwa mara.
Kila la kheri Wana Kimanu manu.

No comments:

Post a Comment