Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Monday, January 26, 2015

Safari ya Matumaini ya Wana Kimanu Manu Yanukia,Maandamano yaanza Rasmi


Shamra Shamra Zimeanza
Safari y matumaini ya African Sports imebakisha KM kidogo
tu ili Ifikiwe,Leo katika Uwanja wa Mkwakwani stadium
Timu hiyo imewafunga timu ya majimaji ya Songea kwa bao
moja kwa bila,Goli lilifungwa na Ramadhani Hamidu kwa kichwa
baada ya kazi ya ziada iliyofanywa na Ali Shiboli,kwa sasa African
Sports inafikisha alama 41 ambapo kwa matokeo
hayo African Sports inahitaji Point tatu tu kupanda ligi kuu ya
soka Tanzania bara almaarufu Vodacom kwani Majimaji atafikisha
alama hizo kwa kushinda mechi zote ikiwemo ya Friends Rangers
wakati Friends Rangers akifungwa na Majimaji atafikisha alama41
kama naye akishinda mechi zake zote,ila Mla mla leo mla jana
kalani.Tayari mguu mmoja wa African Sports upo Ligi kuu Vodacom.
Safi sana wana Kimanu manu.

No comments:

Post a Comment