Timu ya soka ya African Sports ya Tanga Leo tena katika
dimba la Mkwakwani mjini hapa wamewafunga timu ya JKT
MLALE Kwa bao moja kwa bila,Mchezo huo uliokuwa
mkali na wa kusisimua uliwachukua African sports hadi
kipindi cha pili kupata bao hilo la Ushindi baada ya Striker
wao tegemeo Ali Shiboli kumhadaa kipa na mpira uliopigwa na
beki ya African Sports Kutinga wavuni.Kwa matokeo hayo
African Sports wanasubiria mchezo wa kesho kujua hatima yao
ya kupanda Ligi kuu katika michezo miwili kati ya LIPULI NA
KMC Itakayochezwa kesho katika uwanja wa mkwakwani na
mchezo mwengine kati ya FRIENDS RANGERS NA MAJIMAJI
mjini Songea,African Sports Itakuwa na alama 44 ambazo timu tatu
tu kati ya LIPULI,FRIENDS na MAJIMAJI ndio zinazoweza kufikisha.
LIPULI akitoa sare ama kufungwa hawezi kufikisha alama 44,katika
michezo yake mitatu,Majimaji akifungwa ama kutoa sare pia hatafikisha
alama 44,FRIENDS pia ni Vivyo hivyo.HAKUNA JINSI wana
KIMANU MANU wako ligi kuu ya Vodacom..Wacha watuimbie ile
Nyimbo tuipendayo Lazima Tule Kunde..na Kijibwa Koko.
No comments:
Post a Comment