Timu ya Soka ya African Sports almaarufu Wana Kimanumanu
Leo imeendeleza wimbi la ushindi katika ligi daraja la kwanza
inayoondelelea nchini.African Sports ilikuwa nyumbani
ikipepetana na Ashanti United ya Dar-es-Salaam.Goli la African
Sports lilifungwa baada ya Faulu kali kutoka kwa Ali Ahmed Shiboli
ambapo kipa wa Ashanti aliitem na kumkuta Nyanda akaitupia
nyaavuni.Hadi mapumziko African Sports Walikuwa wakiongoza
goli moja,Kipindi cha pili Ashanti waliingia kutaka kusawazisha
lakini African Sports walipata Goli la Pili kwa njia ya Penalti
ambapoa Ali Ahmed aliangushwa kwenye Eneo la hatari,Penalt
ilipigwa na Ali Kagawa.African Sports hadi sasa wamejikusanyia
alama 29 nyuma ya Majimaji ya Songea yenye Alama 31.
Wiki ijayo African Sports inachezwa na Tesema katika Dimba
la Mkwakwani Stadium.
No comments:
Post a Comment