![]() |
| Juan Matta,Wayne Rooney na Radamel Falcao |
Garry Nevvile ambaye kwa sasa ni mchambuzi kwenye kituo kimoja
cha Television Nchini humo amesema Timu yake ya zamani inahitajika
kuongeza nguvu kwenye idara ya Ulinzi na Kiungo kidogo ili waweze
kuendelea kupata matokeo mazuri.Sitashangaa nikiona kocha akiingia
sokoni kuangalia mabeki na viungo kwani ni idara ambayo inayumba
kwa sasa klabuni hapo,Nafikiri kelele nyingi kutoka kwa Van Gaal na
timu kwa ujumla kwa miezi michache iliyopita ni kuendelea kuisuka timu.
Kipaumbele kwa msimu huu ni kucheza Champion League mwakani huku
Van gaal akiahidi Kombe kabla ya Miaka mitatu.Kuhusiana na Champion
ligi mwakani Tayari timu iko kwenye njia sahihi mpaka sasa ila kombe
lazima timu iendelee kusukwa upya tena na tena.Manchester united ina
tatizo la kuumia umia kwa wachezaji wake mara kwa mara hivyo kumfanya
Van Gaal kushindwa kuwa na kikosa chote na machaguo mengi ya wachezaji
kitu ambacho inabidi kitafutiwe ufumbuzi mapema iwezekanavyo,Ushindi
dhidi ya Stoke ungeishuhudia United ikiwa point nne nyuma ya wapinzani
wao Manchester City lakini United ilishindwa kuwafunga Stoke Kipindi
cha Pili cha mchezo,Mwaka uliopita United ilifungwa na Stoke lakini mwaka
huu imetoka na Point huku ikishuhudia washiriki wa Ligi ya mabingwa
Arsenal wakipoteza Point mbele ya Stoke pale Bratania Stadium.

No comments:
Post a Comment