Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Thursday, January 1, 2015

Chelsea Yachapwa Vibaya....Yaongoza ligi kwa Herufi tu

Harry Kane
Mchezaji anayekuja kwa kasi katika ligi kuu ya Uingereza Harry Kane
jana aliwachachafya Vilivyo majirani wao wa jiji la London Chelsea.
Ushindi huo kwa Totenham ulikuwa ni wa kwanza kwa kipindi cha
takribani miaka mitano,Kipindi cha kwanza kilishuhudia Spurs wakitawala
mchezo japo walitanguliwa kufungwa kwa Goli la Diego Costa kabla
Harry kane hajasawazisha na Danny Rose kufunga la pili dakika moja kabla
ya mapumziko,Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Harry Kane tena
akifunga Goli la tatu dakika saba baada ya kipindi cha pili kuanza.Nacer
Chadli alipigilia Msumari wa Mwisho kwa Spurs huku Eden Hazard na
John Terry wakihitimisha idadi ya mabao 3 kwa Chelesea usiku huo.
Kikosi hicho cha Spurs kinashuhudia kikicheza mchezo wa sita bila kufungwa
mara ya mwisho kufungwa ilikuwa dhidi ya Chelsea mwanzoni mwa mwezi
december na Kukwea hadi nafasi ya tano katika msimamo wakiicha Arsenal
nyuma kwa nafasi moja..Kipigo hicho kimewanyima nafasi ya kuongoza
ligi Chelsea huku wakikamatana Point na wapinzani wao wa karibu Man-city
wakiwa wako sawa kwa kila kitu na Chelsea wanaongoza kwa Herufi tu.
Ligi hiyo imesimama kwa siku Tisa kupisha michuano ya Kombe la FA.

No comments:

Post a Comment