![]() |
| Southampton Wakishangilia bao |
waliwachapa bila Hurumu timu yenye kusuasua katika ligi
Arsenal kwa Ushindi wa mabao mawili kwa bila,Alikuwa
ni mshambuliaji hatari wa timu hiyo Sadio Mane alieanza
kupeleka kilio Arsenal na furaha kwa kocha wake Ronad
Komen baada ya makosa binafsi ya ngome inayoonekana
kuvuja ya Arsenal,Goli hilo limemfanya Sadio Mane kufunga
goli la tatu katika michezo miwili iliyopita,
Kutokuelewana kwa mabeki wa Arsenal
kuliwazawadia Southampton goli la pili huku wakishuhudia
mipira kadhaa kutoka kwa Graziano Pelle akipiga post za
pamoja na nafasi kadhaa za wazi ambazo southampton
walizikosa ambazo zingewafanya wakaibuka na ushindi
mnono kuliko huo,lakini haikuwa shida kwani timu ya wenger
haikujitambua mpaka mwisho wa mchezo hivyo watakatifu
wakachukua alama zote tatu za mchezo huo.Kwa ushindi
huo Southampton wamejikita katika nafasi ya nne na kufanya
waendelee kupigania nafasi ya kucheza michuano ya mabingwa
ulaya msimu ujao.Arsenal ambao bado wanasuasua na mashabiki
hawapendezwi na mwenendo wa timu yao mpaka sasa inabakia
nje ya nne bora mpaka sasa.

No comments:
Post a Comment