Mholanzi Luis Van Gaal amesikitishwa na Ratiba Ngumu ya X-Mass
katika ligi kuu ya England,Van Gaal ambaye hii ni mara ya kwanza
kufundisha Klabu ya Ligi kuu England ambayo ndio pekee Ulaya isiyo
na mapumziko ya Xmass kama ligi nyengine barani humo,Van Gaal
alinukuliwa akisema kwamba"Tuna wapendwa wetu,nina Mke,watoto
na wajukuu lakini siwezi kuwa nao X-MASS hii inasikitisha"Sina cha
kufanya kwani nimechagua kuwa mwalimu kwenye Ligi hii,Kucheza,
Kucheza mechi mbili kwa tofauti ya siku mbili sifikiri kama haki kwa
wachezaji,ni ratiba ngumu sana kwa wachezaji na wote wanaohusika
Kocha huyo wa zamani wa Ajax,Barcelona,Bayern Munich na Timu
ya Taifa ya Uholanzi Anakabiliwa na Mechi dhidi ya Newcastle united
Boxing Day,halafu baada ya siku mbili inasafiri kuelekea London
kupambana na Hotspurs kisha itahitimisha Mchezo wake na Stoke city
siku yaa mwaka Mpya na itakuwa siku tatu kabla ya Raundi ya tatu ya
kombe la F.A

No comments:
Post a Comment