Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Tuesday, November 18, 2014

Zilongwa Mbali...Zitendwa Mbali..

Dimba la Mkwakwani Stadium


Nawasabahi wapenzi wa michezo wenzangu popote mlipo
na mnaosoma nakala ya Mgosi wa Sui Sports Zone.Mwaka
2001 pale Mjini arusha wakati bado nikiwa nalisakata
Kandanda Nilikwenda na Timu Vijana ya Eagle kushiriki
mashindano ya East and Central Africa youth champion
yanayokwenda kwa jina la Rollingstone..huko nilikutana
na Mastaa wengi wa Tanzania akiwepo Nyoni Beki kisiki
wa Timu ya Taifa kwa sasa,Siku tulipofika Arusha kama
kawaida ya wachezaji na hii ni Duniani kote ni ile hamasa
ya kutaka kuona sehemu ya Tukio(Uwanja) wa mashindano,
tukaenda Sheikh Amri abeid Kaluta na kuingia uwanjani na
kuanza kuelekea sehemu ya kuchezea na Mokasini zetu za
 sikukuu mara tukasikia sauti ya kizee ikituita..aloo..aloo
 

Kilimanjaro Wakiwa wameweka Jukwaa Uwanjani


tulipogeuka tukapewa ishara ya kuitwa mahali Fulani pale
uwanjani,tukasalimia yule mzee na akajitambulisha yeye
ni meneja wa uwanja akatuuliza kulikoni mnaelekea uwanjani?
tukamjibu tukiwa tunajiamini kabisa sisi ni vijana kutoka Tanga
tumekuja kwenye mashindano ya Vijana yanayoanza kesho,
tunataka kuona sehemu ya kuchezea,akatuangalia juu mpaka
chini halafu akatujibu sio ruhusa kuingia uwanjani kiholela subirini
 mkija kucheza mtaingia kiwanjani kama kwa mbali hamridhiki
kuona uwanja subirini kesho,Tukashangaa na tukafikiria ni utani
na yule mzee akaendelea na shuhuli zake ndipo tulipojua kamaanisha
alichokisema na tulipokwenda majukwaani ki ukweli hatukuona
 mtu akikatiza kiwanja na Mokasini,Kesho yake kama kawa kikapigwa
 na Tulitoka suluhu,Lengo la kuwaletea Makala haya ni kuelezea
masikitiko yangu kwa jinsi hadhi ya viwanja zilivyoshuka kwa sasa
 nchini Tanzania,huhitaji njumu kuingia uwanjani unahitaji Mokasini
 uingie kiwanjani na hadhi hiyo miongoni mwa watu wa kubwa
wanaoshusha ni wale wale wenzetu kwenye sekta ya michezo,
 

Maandalizi ya Kinywaji Uwanjani


Serengeti Ambao ni wadhamini wa Taifa Stars,na Kilimanjaro
wadhamini wa Klabu zenye mashabiki wengi Tanzania Simba na Yanga
 kasoro Mimi tu ninayeandika Makala haya,Hawa jamaa kila mwaka
wanaandaa matamasha ya kimuziki makubwa sana na hawayapeleki
 kokote isipokuwa katika viwanja vya mpira lakini hao hao ni mabingwa
 wa kuponda viwanja vibovu pindi ligi kuu inapoanza sijui tuwaelewe
 vipi kiukweli,watu wanajazana katikati ya kiwanja na siku iwe
kulinyesha mvua ndio utakapojua uwanja ni Zizi la N’gombe ama
uwanja wa kuchezea mpira,hivi wana maana gani tuseme?
hakuna sehemu nyengine ya kufanya matamasha yao mpaka
waingie kiwanjani?kama wanaona ni muda wa kupromoti starehe
 si wajenge kumbi sasa za Starehe?wasitumie madhaifu ya chama
tawala kuwapa kiwanja ndio na wao watuharibie viwanja vya mpira,
watu wa mpira walikaa wakaona wajenge viwanja vya mpira na watu
 wa Muziki wakae wajenge maholi ya muziki sio kuchanganya madawa,
 

Meza za Chakula na Vinywaji Uwanjani


vipo viwanja vingi vya wazi kwa hadhi yao na pesa walizonazo wangeweza
 kurekebisha na kupigia miziki huko lakini wana ulazima wa kuingia kiwanjani
 na Kinachosikitisha wao ni wadau wakubwa wa Mpira,nafikiri wanajidai wadau
 wa Mpira ila ni wanafiki ki ukweli,zama za Kutokuingia kiwanjani na Mokasini
zimepitwa na wakati sasa,huhitaji Njumu kuingia Dimbani,Vaa katambuga,
pekupeku,malapa,mchuchumio unaweza ingia dimbani kulisakata Dansi na
 wengine inafikia pia kufanya viwanja hivyo Vyumba vya kulala kwa kufanya yao.
Tulisubiria sana kuingia kiwanja cha mpira wakati wa utoto wetu lakini kipindi hiki
 hakuna cha kusubiria,siku na saa yoyote unataka kuingia kiwanjani utaingia tu
hakuna wa kukuzuia,sio sehemu maalumu tena ni sehemu ya kawaida na ya
kijamii kama masoko ambayo unaweza kuinga hata bila kununua kitu na usiulizwe,
Halafu na nyie wamiliki wa Viwanja basi njaa zisiwaue hivyo,kwani wanamipa
shilingi ngapi?siamini kama wanatoa pesa ya maana hivyo kama tunazotoa sisi
watu wa mpira pindi tukicheza mpira hapo kiwanjani,Mechi moja ya Coastal na
 Yanga pale Mkwakwani stadium Uwanja walipata takribani milioni 18,


sidhani na siamini kama Hao Serengeti na Kilimanjaro wanatoa hata asilimia
 kumi ya hiyo hela,sasa mbona watu wa uwanja mnatuangusha kwa vijisenti
 vya mara moja kwa mwaka?uwanja ukifungiwa hizo hela zitapatikana wapi tena?
namalizia na maneno ya wahenga yanayosema”Msiache mbachao kwa msaada upitao”
 
National Stadium

No comments:

Post a Comment