Timu ya soka ya African Sports ya Mjini Tanga
maarufu wana Kimanu manu leo katika uwanja
wake wa Nyumbani ilitoa suluhu kwa kufungana
mabao moja kwa moja na timu ya Friends Rangera
katika Mchezo mkali wa vuta nikuvute katika dimba
la Mkwakwani,Ilikuwa ni Friends Rangers ndio
walifanikiwa kujipatia Goli la kwanza katika kipindi
cha kwanza cha Mchezo huo na kuwavunja nguvu
African sports mbele ya mashabiki wao,Hadi mapumziko
Friends Rangers walikuwa Mbele kwa Goli hilo moja,
Kipindi cha Pili kilianza kwa kasi kwa African Sports
kulisakama Goli la Friends Rangers,African Sports
walisawazisha Bao katika Dakika ya 84 ya mchezo huo
kupitia maulidi na kuwapa ahueni ya kuokota walau
point moja katika Mchezo huo,hadi mwisho wa Mchezo
Friends Rangers 1-African Sports Moja na kuwafanya
Friends kujikusanyia jumla ya alama 20 katika Michezo
11 huku African Sports wakiwa na alama 17 katika
michezo 10 kwani kuna kipora kati yake na Villa Squad
Kitakachochezwa Jumamosi week hii,Ligi hiyo inaendelea
Kesho kwa Villa Squad Kupambana na TESEMA ambao
wanautumia Uwanja wa Mkwakwani kama uwanja wa
Nyumbani..
No comments:
Post a Comment