Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Sunday, November 16, 2014

Eagle Academy Yaiadhibu Moa Original

Timu ya soka ya Eagle Academy ya Tanga leo
katika mchezo wa Ligi daraja la Tatu mkoa wa
Tanga imeiadhibu Timu ya Moa Original kwa
Bao moja kwa bila katika mchezo mkali na wa
kuvutia,Mchezo huo ulianza majira ya Saa nane
mchana,Bao hilo lilifungwa na Mshambuliaji
hatari wa Eagle Academy HERBERT MHINA
Ama wanamuita Herbert Magoli,na kumfanya
kufikisha magoli matano tokea ligi hiyo ianze,
hiyo ilikuwa Round ya kwanza ya ligi hiyo ya
mkoa wa tanga huku Eagle ikiwa na alama sita
mpaka sasa,
Katika mchezo mwengine timu ya Jeshi
worriers iliiadhibu vikali timu ya Gurudumu kwa
mabao Tisa kwa Mbili.

No comments:

Post a Comment