MSHAMBULIAJI
Lionel Messi amevunja rekodi ya mabao Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya
kufunga hat-trick jana katika ushindi wa 4-0 dhidi ya APOEL mjini
Nicosia na kufikisha jumla ya mabao 74 kwenye michuano hiyo.

Nyota
huyo wa Barcelona alimfikia mchezaji aliyekuwa anaongoza, Raul baada ya
kufunga mabao mawili dhidi ya Ajax mapema Novemba, lakini mabao yake
matatu ya jana yanamfanya awapiku wote.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari baada ya mechi Messi amesema: "Nina furaha sana
kuvunja rekodi hususan katika mashindano muhimu kama haya, lakini huu
ulikuwa mchezo mkubwa kwetu mbali na rekodi zote,"amesema. Mchezaji huyo mzaliwa wa Argentina na aliyekuzwa kisoka Barcelona tayari ana Rekodi ya Kuwa Mfungaji bora wa wakati wote Barcelona na katika Ligi ya Mabingwa anafuatiwa kwa Ukaribu na Cristian Ronaldo mwenye mabao 69 mpaka sasa kwa wachezaji ambao bado wanacheza Kandanda

Lionel Messi akishangilia baada ya kutimiza mabao 74 kwenye Ligi ya Mabingwa
No comments:
Post a Comment