Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Thursday, November 27, 2014

Arsenal Yakata Ticket Ya Kutoshiriki Mabingwa Mwakani


WASHIKA Bunduki, Arsenal wamefuzu kuingia hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya Borussia Dortmund Uwanja wa Emirates katika mchezo wa Kundi.
Yaya Sanogo aliifngia Arsenal bao lake la kwanza kwenye mechi ya mashindano dakika ya pili, ingawa kinda huyo Mfaransa alionekana kama alikuwa ameotea.
Alexis Sanchez akaifungia timu ya Arsene Wenger bao la pili dakika ya 57 na kuihakikishia kuingia hatua hiyo ya mtoano.Kwa matokeo hayo kwa sisi Tunaoijua Arsenal na kwa hali ilivyo ligi ya England Arsenal amejikatia Ticket y kutoshiriki ligi ya Mabingwa mwakani kwani mpaka sasa wanashika nafasi ya Nane na jinsi wanavyoshindwa kuendana na Michezo mingi kwa wakati mmoja ni wazi watakosa nafasi hiyo mwakani,Muda ndio utaongea
Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Martinez, Chambers, Mertesacker, Monreal, Gibbs, Arteta/Flamini dk66, Oxlade-Chamberlain/Campbell dk89, Ramsey, Cazorla, Sanchez, Sanogo/Podolski dk78.
Borussia Dortmund; Weidenfeller, Piszczek, Subotic, Ginter, Schmelzer, Gundogan, Bender, Grosskreutz, Immobile/Kagawa dk60, Mkhitaryan na Aubameyang/Ramos dk60. 
Alexis Sanchez runs towards the Arsenal fans in celebration of his second half strike against Borussia Dortmund
Alexis Sanchez akikimbia kushangilia baada ya kuifungia Arsenal bao la pili dhidi ya Borussia Dortmund
Sanogo shoots past Dortmund keeper Weidenfeller (right) to score the opening goal of the game
Sanogo akifumua shuti kumtungua kipa wa Dortmund, Weidenfeller (kulia) kuifungia Arsenal bao la kwanza

No comments:

Post a Comment