MANCHESTER City imeshinda mabao 3-2 dhidi ya Bayern Munich katika mchezo wa Kundi E Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Etihad.
Sergio
Aguero alifunga mabao mawili dakika za mwishoni ili kuipatia
ushindinhuo Manchester City, ambao sasa wanafufua matumaini ya kufuzu
hatua ya mtoano ya michuani hiyo.
Aguero
aliifungia bao la kuongoza City dakika ya 21 kwa penalti iliyomponza
Mehdi Benatia kutolewa kwa kadi nyekundu kwa rafu aliyocheza.
Bayern Munich ikatoka nyuma na kupata mabao mawili yaliyofungwa na Xabi Alonso dakika ya 40 na Robert Lewandowski dakika ya 45.
Lakini shukrani kwake Aguero aliyeifungia City dakika ya 85 na 90 kukamilisha hat trick yake jana.
City
sasa itasafiri kuwafuata Roma kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa kundi
hilo Jumatano ya Desemba 10 ikihitaji ushindi ili ifuzu.
Kikosi
cha Manchester City kilikuwa; Hart, Sagna/Zabaleta dk68, Kompany,
Mangala, Clichy, Fernando, Milner/Jovetic dk66, Jesus Navas, Lampard,
Nasri na Aguero/Demichelis dk94.
Bayern
Munich; Neuer, Rafinha, Benatia, Boateng, Bernat, Alonso, Hojbjerg,
Rode/Dante dk25, Robben, Lewandowski/Shaqiri dk84 na
Ribery/Schweinsteiger dk81.
Sergio Aguero akikimbia kushangilia baada ya kuifungia hat-trick Man City jana dhidi ya Bayern Munich
No comments:
Post a Comment