Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Saturday, November 15, 2014

Safari ya matumain ya Wana Kimanu manu Bado iko sawai

Timu ya soka ya African sports ya Tanga almaarufu
wana Kimanumanu leo waliichabanga bila huruma
timu ya Kurugenzi Iringa pamoja na Uchovu wa safari
ndefu kutokea Songea na inaripotiwa waliingia jana usiku,
Timu ya Kurugenzi ndio ilikuwa ya kwanza kuuona mlango
wa African Sports kipindi cha kwanza lakni iliwachukua
muda Mfupi wana kimanumanu kusawazisha bao hilo
kwa nia ya penalt baada ya mshambuliaji wa African sports
kukwatuliwa katika eneo la Penalt,Wana kimanu manu
waliendelea kulisakama lango la Kurugenzi na kufanikiwa
kujipatia bao la pili muda mchache kabla ya mapumziko,
Hadi kipenga cha mwisho African Sports 2 kurugenzi 1.
Wana kimanumanu watajitupa tena uwanjani siku yya jumatano
katika uwanja huo wa Mkwakwani mjini hapa,Kila la kheri
Kimanu manu kila la kheri Tanga

No comments:

Post a Comment