RONALDO AING'ARISHA REAL MADRID LIGI YA MABINGWA ULAYA
BAO
pekee la Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo limeipa ushindi wa
1-0 ugenini Real Madrid dhidi ya FC Basle katika mchezo wa Kundi B Ligi
ya Mabingwa Ulaya usiku huu.
Mreno
huyo, aliyeondoka Manchester United kutua Madrid kwa dau la rekodi,
alifunga bao hilo pekee muhimu dakika ya 35 akimalizia kazi nzuri ya
Mfaransa, Karim Benzema.
Real
Madrid sasa inaongoza Kundi B kwa rekodi nzuri ya ushindi, huku ikiwa
imesaliwa na mechi moja, wakati kwa kipigo cha leo, Basle hatima yao
itajulikana baada ya mechi ya mwisho dhidi ya Liverpool kama watasonga
mbele au, la.Cristian Ronaldo kwa bao hilo atakuwa sawa na Raul Gonzalez katika Rekodi za wapiga mabao wa muda wote katika mashindano hayo ya Ligi ya mabingwa Ulaya na Nyuma ya Hasimu wake Lionely Messi kwa mabao matatu ambaye juzi alipiga Hattrick kwa Barcelona,Messi ana Mabao 74 na anasadikiwa kuongeza mabao hayo kwani bado anacheza yeye na Ronaldo.
Kikosi
cha Basle kilikuwa; Vaclik, Degen/Hamoudi dk76, Schar, Suchy, Safari,
Elneny, Frei/Diaz dk83, Zuffi/Kakitani dk87, Gonzalez, Embolo na Gashi.
Real
Madrid: Navas, Arbeloa, Varane, Ramos, Coentrao, Kroos, Isco/Nacho
dk93, Rodriguez/Marcelo dk89, Bale, Ronaldo na Benzema/Illarramendi
dk71.
Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia bao pekee Real Madrid
Gareth Bale wa Real Madrid akipambana na beki wa Basle, Philipp Degen
No comments:
Post a Comment