Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Thursday, November 27, 2014

Majogoo wa Liverpool Wanazidi KUCHECHEMEA

LIVERPOOL imelazimishwa sare ya 2-2 na Ludogorets katika mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu.
Wenyeji, Ludogorets walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Dani Abalo dakika ya tatau, kabla ya Liverpool kusawazisha kupitia kwa Rickie Lambert dakika ya nane.
Wekundu wa Anfield walipata nao lililoelekea kuwa la ushindi kupiti kwa Jordan Henderson dakika ya 37 kabla ya Georgi Terziev kuisawazishia Ludogorets dakika ya 88.Timu hiyo ya Jiji la Liverpool wanazidi Kupoteana kila Uchao kwa kuwa matokeo yasiyoridhisha mpaka kufikia kutaka kutimua Kocha.
Kikosi cha Ludogorets kilikuwa; Stoyanov, Junior Caicara, Moti, Terziev, Minev, Misidjan, Dyakov, Fabio Espinho/Younes dk80, Mihail Aleksandrov/Wanderson dk72, Marcelinho na Dani Abalo/Quixada dk69.
Liverpool: Mignolet, Johnson, Skrtel, Toure, Manquillo, Henderson, Gerrard, Lucas, Lambert, Allen na Sterling/Moreno dk82.
Liverpool's Steven Gerrard and Rickie Lambert  look dejected after George Terziev (not pictured) scored for Ludogorets
Wachezaji wa Liverpool, Steven Gerrard na Rickie Lambert wakiwa wanyonge baada ya George Terziev (hayupo pichani) kuisawazishia Ludogorets

No comments:

Post a Comment