Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Sunday, November 23, 2014

Wanakimanu Manu Safi sana......Safari ya Matumaini






Timu ya soka ya African Sports ya Tanga almaarufu Wana Kimanumanu
leo imewapa raha wapenzi wa Tanga  kwa kuibanjua Villa Squad mabao
mawili kwa Moja katika Mchezo mkali na wa Kusisimua uliopigwa
katia uwanja wa Mkwakwani ,Ilikuwa ni African Sports ndio walioanza
kupata bao kupitia Mshambuliaji wake mahiri Hassan Mtemera 
"Gurudumu"na  Villa Squad walifanikiwa kusawazisha kabla ya mapumziko
na mpaka mapumziko African Sports 1 Villa Squad 1.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo African Sports walilisakama
lango la Villa squad hadi wakafanikiwa kupata goli la pili,
kwa ushindi huo African Sports wamefikisha Alama 20 na kushika nafasi ya 
Nne na wamefungana alama na Lipuli ya Iringa huku Friends Rangers akiwa na 
alama 21 na maji maji anayeongoza ligi akiwa na alama 24 mpaka round ya kwanza inaisha,
Kila la kheri African Sports

No comments:

Post a Comment