Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Saturday, October 4, 2014

Wagosi watoa Burudani Mkwakwani,Ndanda Alala na Viatu

ndanda katika Nembo yao
 Hayawi hayawi yamekuwa leo katika uwanja
wa Mkwakwani mjini Tanga Wagosi wa Kaya
Coastal Union Wamewapa Raha mashabiki
wake kwa kuwachapa bila huruma Ndanda FC
Kwa kichapo cha bao mbili kwa Moja,
Mfungaji wa Bao la kwanza MAHUNDI


Mashabiki wa Ndanda walianza kuingia Tanga
kunako saa sita mchana kwa Mabasi matatu
kwa Tambo na Nyimbo wakiwa na hakika ya
Ushindi,Coastal Union hawakuwapa nafasi
Ndanda FC Kushangilia timu yao kwani
waliandika bao lao katika dakika ya kwanza ya
mchezo huo,
Ramadhani Salimu akiweka Faulu
 Ndanda walichanganyikiwa kitendo kilichofanya
kocha wao mkuu kusimama na kuanza kutoa
maelekezo baada ya awali kocha msaidizi kuwa
ndio muelekezaji,Coastal hawakubaki nyuma
kwa kuendelea kusukuma mashambulizi yao
kwa ndanda na yalizaa matunda kwa kuandika
baola pili muda mchache kabla ya mapumziko
Heka heka langoni mwa Ndanda
Bao lililowekwa kimiani na Tumba swedi na kuumaliza
mchezo huo kabisa na kwafanya washabiki wa Ndanda
kushindwa kuendelea kuimba Nyimbo zao walizoandaa
Kocha wa Ndanda na Refarii wa akiba aliyekuwa na Bendeji                                                                                                                                                                                                                                                                      
mchezo huo uligubikwa na matokeo tofauti tofauti kwa washabiki
 wa Ndanda kumpiga jiwe refa msaidizi wa mchezo hali iliyofanya 
mchezo kusimama kwa takribani dakika sita kusubiria refarii huyo kutibiwa,Matukio
 mengine ni Coastal union kuwa na mashabiki wa Asili ambao 
 walivaa jezi za mdhamini wa zamani Binslum Sound badala ya mdhamini huyu wa 
sasa Pembe,Mchezo unaofuata 
Coastal wanacheza na Mgambo Shooting ambao kesho 
wao wana Kibarua kigumu cha kupambana na wakata 
Miwa wa Mtibwa Sugar,Ahsante wagosi kwa kuwatuliza 
wamakonde wangesumbua sana leo hapa Mkwakwani,na 
Kila la kheri Mgambo Shooting,tupeni raha walizotupa 
Wagosi wa Kaya Coastal Union


No comments:

Post a Comment