| Mchezaji Wa African Sports na Jezi yenye Udhamini |
almaarufu wana Kimanumanu Jana waliendelea
kuwapa raha mashabiki wao wa mjini hapa kwa
kutoa kichapo cha Bao Moja kwa Bila dhidi ya
Panone katika Mchezo mkali na wa Kusisimua,
Katika Mchezo huo uliokuwa wa Vuta nikuvute
kabla ya kuanza kulikuwa na hali ya sintofahamu
kwa Jezi za timu hizo kufanana lakini African
sports wakaonyesha kuwa wao Umaskini basi
walianza kuvaa Jezi nYeupe yenye Udhamin
wa aliyekuwa Mdhamini wa Coastal Union
Nassoro bin Slum kisha wakazivua na kuvaa
za Blue zisizo na Mdhamini kwani Panone walikua
na jezi nyeupe pia.
| Mussa Chambega akiwa katika heka heka |
kwa kipindi kizima cha kwanza Ndipo
walipoingia na Jezi nyengine za Blue Zenye
udhamin wa Binslum hivyo kuibua shangwe
kwa mashabiki walioikuwepo uwanjani hapo,
Hali hii ni dalili njema kwa wana Kimanumanu
hususani kwa wapenzi wanaoijua Timu hiyo
huko nyuma kama jezi zingegongana
wasingekuwa na jeuri ya kubadili Jezi mara
tatu kwani hawakuwa na kitu,lakini sasa mambo
yanaonekana yamewabadilikia sana kiasi cha
timu inayosifika kwa pesa kama Panone kuonekana
ni ya kawaida tu Kwa African Sports .
| Rashid Mbu |
kwa African sports kuadika bao lake la kwanza
kwa mkwaju wa Penalt baada ya wachezaji wa
panone kumkwatua Gurudumu katika eneo la
hatari ndipo Mendi akakwamisha mkwaju huo
na Goli hilo linazidi kuwapa African Sports
Ushindi wa Asilimia Mia katika Mechi zake za
kirafiki,ikumbukwe week iliyopita waliwafunga
JKT Oljoro kwa bao moja kwa Bila.
| African Sports wakipiga mkwaju wao wa Penalt |
mwaka huu na mwezi huu wa kumi inajipanga vema
kuhakikisha wanapanda daraja baada ya kukaa chini
kwa takribani Miongo miwili,Mchezaji wake wa Kushoto
Issa hajawahi kuiona Timu hiyo ikiwa ligi kuu hivyo
anasikia tu hadithi za watu,Baada ya mchezo huo
mashabiki wa African Sports hawakuacha Tambo
kwa kuwabeza watani wao wa Jadi Coastal union
kwamba Nyie mliona cha nini sisi tuliona tutakipata
lini wakimaanisha Mdhamini wao Mpya Nassoro
Bin Slum,Hata hivyo udhamini huo haukuwekwa wazi
nipaka yake,Kila la Kheri African Sports kwenye
ligi ngumu ya Kupanda daraja
No comments:
Post a Comment