Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Sunday, October 12, 2014

Hivi TFF Wanajua kama Kuna wachezaji Ligi Daraja la Kwanza?

Ligi ya Soka Daraja la Kwanza imeanza Rasmi Jana
katika Viwanja tofauti tofauti Husussani vyenye Timu
Shiriki ya Ligi hiyo,Leo hapa tanga Tunashuhudia timu
mbili zenye majina Pacha zikiumana Vilivyo katika
Dimba la Mkwakwani Stadium,Africana Sports ya Tanga
na African Lyon ya Dar-es-salaam,Mchezo unaosubiriwa
kwa hamu na wakazi wa Tanga na Vitongoji Vyake.
Wito kwa wadau wa soka ni kuhusiana na Chama cha
Mpira wa Miguu Tanzania TFF Kuangalia ligi hiyo kwa
jicho huru kwani ni kipindi muafaka kupata wachezaji wa
Timu ya Taifa ya Tanzania TAIFA STARS ambayo inasuasua
kwa sasa badala ya kutupia jicho ligi moja tu ya Vodacom
kupata wachezaji wa Timu hiyo,Mwanzoni mwa mwaka huu
 tulishuhudia Uongozi wa Shirikisho hilo ukija na Mpango
mkakati wa Maboresho ya Taifa Stars Mpango ambao
uliwakusanya Vijana takribani Mia Tatu Nchini ili kuona
kama kuna uwezekano wa Kuonyesha vipaji vitakavyowafanya
waweze kushiriki katika Timu ya Taifa,mpango ambao wadau
wengi w Mpira waliuita mpango wa Zimamoto kwani Kijana
aliheza dakika 45 ili kuonyesha kupaji hali amabayo kiuhalisia
haiwezekani mchezaji kupatikana ndani ya Dakika 45 za
Mchezo wa Soka japo mara Chache sana inatokea,Mpango
huo uliteketeza Mamilion ya Shilingi na Haukufanikiwa kabisa
japo wahusika wako kimya katika hilo,
Ni vema sasa TFF Wakatumia nguvu kidogo kwa kuweka
watu wakachagua wachezaji wa Timu ya Taifa kwa Vilabu hivi
vya daraja la kwanza kwani kutakuwa na mechi nyingi
zinazotosha kuona uhalisia wa mchezaji...KILA LA KHERI
AFRICAN SPORTS KILA LA KHERI TANGA

No comments:

Post a Comment