Team ya Soka ya African sports ya Mjini Tanga
jana ilifanya Kufuru baada ya Kuibamiza Timu ya
Mandingo Veteran kwa Idadi kubwa ya Mabao
Nane kwa Bila 8-0,katika Mchezo ambao
ulifanyika jana katika uwanja wa Mkwakwani
majira ya saa Kumi jioni,Team Hiyo ya African
Sports inayojiwinda katika Kinyang"anyiro cha
michuano ya Ligi Daraja la Kwanza inayotarajiwa
kuanza kesho katika viwanja mbali mbali Nchini
ilicheza mchezo huo wa kujipma Nguvu na wa
Mwisho kabla ya ligi kuanza,Kocha wa timu hiyo
alikuwa mwenye furaha kwani alikuwa anajaribisha
mifumo mbali mbalia atakayoitumia katika ligi na
yote imeonekana wachezaji wameielewa,Timu hiyo
ambayo tokea mwaka huu uanze hawajawahi kufungwa
hivyo kujiwekea Historia ya Asilimia Mia moja
ushindi,Kila la kheri African Sports kila la Kheri Tanga
Inshallah Tutapanda...
No comments:
Post a Comment