Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Saturday, September 27, 2014

Tanga Mambo si Shwari,Mgambo na Coastal walala katika Ligi ya Vodacom

Bakari Shime Kocha Mgambo akitoa maelezo


Katika Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga
palikuwa na patashika nguo kuchanika wakati
timu ya Mgambo Shooting ilipokuwa ikipepetana
na Stand united ya Shinyanga,Mchezo huo ulianza
majira ya saa kumi kamili jioni kwa timu zote kucheza
mchezo wa Kutegeana tegeana na Ufundi mwingi
Mgambo wakipata Maelezo
Iliwachukua Stand United hadi dakika ya 13
ya Mchezo kuandika bao la kwanza kwa
uzembe wa Beki wa Mgambo Aliyekosea
kuundoa mpira katika hatari hivyo Mchezaji
wa Ndanda akaupitia na kumpasia mfungaji
Musa Mohamed nae bila ajizi akapasia Nyavu
Mfungaji wa Bao la Ndanda mwenye namba 20

 na kuamsha shangwe kwa mashabiki wachache
wa Stand walioambatana na timu hiyo kutokea
Shinyanga,Mgambo walifanya Mabadiliko kadhaa
ili kuweza kujinusuru kwa kuwaingiza Mohamed
na kuntoa Samata,halafu walimtoa Ayoub na
kumuingiza Boli lakini mabadiliko hayo hayakuzaa
matunda
hivyo hadi mwisho wa mchezo Stand United 1 Mgambo
shooting hawakupata Kitu,
Kocha wa Ndanda akitoa maelezo
Kwingineko Kule Mjini Mbeya Timu ya
wagosi wa kaya ya Tanga ilipokea kipigo
cha bao moja kwa bila,Bao lililofungwa kwa
 Njia ya Penalt ya Kitatanishi....Week ijayo
Mgambo wanaelekea Manungu Morogoro
huku Wagosi kwa mara ya kwanza wanakuwa
katika uwanja wao wa Nyumbani
Mkwakwani Stadium.

No comments:

Post a Comment