Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Sunday, September 21, 2014

Wagosi waanza KUFANYA YAO

Tanga raha Imeingia tena leo baada ya jana
kushuhudia timu ya Mgambo Shooting ya
jijini hapa ikiifunga bila huruma timu ya Kagera
sugar leo tena wakazi wa Tanga na Vitongoji
vyake wamezidi kupata raha kwa Timu yao
kipenzi Coastal Union Mangushi,Wagosi wa
Kaya ikiikatalia katu katu timu ya Simba sports Club
kuondoka na Point tatu katika mchezo mkali na
wa kusisimua uliopigwa katika Dimba la Taifa
Ilikuwa ni simba sports club waliojipatia mabao
yote matatu katika kipindi cha kwanza kabla ya
Coastal union kuanza kusawazisha moja baada ya
jingine na kufanya matokeo kuwa mbili kwa mbili
hadi muda wa mwisho wa Mchezo huo.
Timu ya Coastal baada ya hapo wataanza safari
kuelekea Mbeya kupambana na Mbeya City
timu ambayo ilikuwa na Vishindo katika ligi iliyopita
lakini Coastal Iliwasambaratisha mara zote walizokutana
Kila la Kheri Wagosi tena kule Mbeya,huku
tukiwasubiria Stand hapa Tanga na Mgambo
Shooting ambapo tunaamini Mgambo itashinda
na Kurejesha heshima ya Mpira wa Miguu katika
jiji hili la Tanga.

1 comment: