Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Sunday, September 21, 2014

Manchester United Bado Gonjwa Gonjwa

Ligi kuu ya Nchini England imeendelea Leo
kwa Mechi mbili,mechi ya kwanza ilikuwa
baina ya Leicester City Dhidi ya Manchester
 United,ilihali Mechi ya pili ilishuhudia
timu mbili zinazopewa nafasi ya Ubingwa
kati ya Chelsea na Manchester City.
Tukianzia katika jiji la Leicester Mchana wa
leo umeshuhudia Timu iliyopanda daraja ya
Leicester City ikitokea Nyuma na kuibamiza
Bila huruma Timu ya Manchester United kwa
mabao Matano kwa matatu na kudhihirisha
kuwa Manchester United bado ina Kazi Ngumu
ya kujibabadua kutokea kuwa timu isiyotisha
na kurudia enzi zake ya kuwa moja ya timu kigogo
nchini England.Manchester united ilishuhudia nyota
wake Angel Dimaria akiumia katika kipindi cha
kwanza cha Mchezo huo,Kwingineko kulikuwa
 na mtanange wa kukata na shoka kati ya Manchester 
city dhidi ya Chelsea ambayo matokeo yaliisha
kwa sare ya magoli moja kwa moja,Goli la
Chelsea lilifungwa na ANDRE SCHURLE wakati
la kusawazisha la Manchester city lilifungwa na
mchezaji mkongwe wa Chelsea Frank Lampard
ambaye baada ya kufunga goli hilo hakushangilia
kutokana na kuonyesha heshima kwa Timu hiyo
yake aliyoichezea kwa zaidi ya Muongo Mmoja

No comments:

Post a Comment