Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Friday, September 26, 2014

Wana Kimanu Manu Wafanya Yao Mkwakwani katika maandalizi ya Kucheza Ligi kuu mwakani

Timu ya Soka ya African Sports ya Tanga
jana iliwachapa Bila huruma timu ya JKT
Oljoro kwa Bao moja kwa bila katika
mchezo wa Vuta nikuvute wa Kirafiki
uliofanyika katika Uwanja wa Mkwakwani
mjini Tanga,Katika Mchezo huo wa Kujipima
nguvu uliochezwa Jana Jioni Ulishuhudia timu
hizo zikicheza Kandanda safi muda wote wa
mchezo hali iliyopelekea washabiki kutokujua
nani ataibuka mbabe katika Mchezo huo,
Kikosi cha JKT OLJORO








Iliwachukua African sports iliyokuwa ikishangiliwa
na umati wa amashabiki wake kwa Ngoma na
Mbwembwe kama Jadi ya timu hiyo ilivyo
kushangilia bila kuchoka hadi dakika ya 76 ya
mchezo huo kwa Goli safi baada ya beki wao
wa Upande wa kulia kuambaa ambaa na Mpira
na kupiga Krosi safi iliyopelekea Kipa wa JKT
Oljoro kuitema na kumkuta Mfungaji wa Goli hilo
lililofungwa na Nahodha wa Timu Hiyo Mendi.
African Sports wakishangilia Bao lao


Timu ya JKT Oljoro walijitahidi kadiri ya uwezo wao
kulisawazisha bao hilo lakini juhudi zao hazikuzaa
matunda Mpaka firimbi ya mwisho ya Muamuzi
Ibrahimu Kidiwa kuashiria Mwisho wa Mchezo huo,
ikumbukwe Timu hizo zinajiwinda kushiriki ligi daraja
la kwanza inayotarajiwa kuanza kutimua Vumbi mwezi
ujao,JKT Oljoro ambao walishuka Daraja watakuwa
kundi tofauti na wana Kimanumanu,Kila la kheri
AFRICAN SPORTS,Kila la kheri Jiji la TANGA.

No comments:

Post a Comment