imeahidi wapenzi wake wa Mjini humu kutokuwa na
mashaka katika mechi yao wanayotarajiwa kukutana
na Timu inayotangazwa vyema na Magazeti nchini
Mbeya City,Timu hizo zinatarajiwa kukutana katika
mchezo mkali na wa kusisimua utakaochezwa katika
uwanja wa Kumbukumbuku ya Sokoine kesho siku
ya Jumamosi majira ya saa kumi Jioni,Ikumbukwe
timu hizo katika michezo yao ya kwanza Zilitoka suluhu
uku Coastal Union wakitoka suluhu na Simba Sports
Club ya Dar-es-salaam kwa kutoshana nguvu ya mabao
2-2 katika mchezo mkali na wa kusisimua ambapo
ilishuhudia Wagosi mara zote wakisawazisha mabao
yaliyofungwa na Simba,wakati Mbeya city nayo
ilitoka suluhu uwanja wake wa Nyumbani hivyo
kuufanya mchezo huo kukutanisha timu zenye point
moja moja.
![]() | |
Washabiki wa Coastal wakishangilia baada ya Kuibwaga | Mbeya city Msimu uliopita |
Msimu uliopita ikumbukwe wagosi ni
moja ya timu iliyokataa kata kata kufungwa na timu
ya Mbeya city iliyoanza kwa kishindo ligi hiyo na
kunyanyasa timu nyingi lakini sio Wagosi ambapo
katika mchezo wa kwanza walitoka suluhu na Mchezo
wa pili Mbeya city waliangukia Pua kwa Kupokea
kichapo cha Mabao mawili kwa Bila,Kingine kikubwa
katika mchezo huu ni kuhusu Mdhani wa zamani wa
Wagosi wa kaya kwa sasa anaidhamini Timu ya Mbeya
city hivyo kutakuwa na hali ya kupimana Mbavu.
No comments:
Post a Comment