Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Tuesday, September 16, 2014

Safari na Muziki....reubenpaul nenda mwanangu

Uko pouwa Totooooo?
reubenpaul:achana na mimi.
Mimi:yamekuwa hayo tena hata usemeji safari unayo..
reubenpaul:ni kilometer ngapi kutokea hapa?
Mimi:kama kilometer 80 hivi
reubenpaul:Utatembea kwa muda gani?
Mimi:Lisaa limoja
reubenpaul:una namba ya trafic?
mimi:ya nini namba ya trafic
reubenpaul:nataka kuulizia habari za sheria za barabarani,
hujafunga mkanda,speed yako siiamini,na pia nataka
kujua sheria ya mtoto kukaa mbele bila Kiti chake?
mimi:wakiitwa watoto na wewe utatoka?
reubenpaul:Naweza kuona licence yako kabla safari haijaanza?
Mimi:Kaa kimya nataka kulianzisha,tazama mizigo yako yote ipo hapo nyuma?
Reubenpaul:Mbona mama simuoni hapa
Mimi:mama yako ni mke wangu we anakuhusu nini?
Reubenpaul:mzee we Ninyanyase tu ila Utanikumbuka
Mimi:nenda wewe...Chombo kikawaka Safari ikaanza

1 comment: