kwa Jina la Vodacom Premier League
Inatarajia kuanza Kutimua Vumbi Kesho katika
viwanja mbali mbali Nchini,Hapa Mjini Tanga
timu ya Mgambo shooting ya Kabuku handeni
itamenyana na timu ya Kagera sugar ya kule nchini
Bukoba katika uwanja wa CCM Mkwakwani.
wakati timu nyengine kutoka Tanga Wagosi
Coastala Union watatupa karata yao kesho kutwa
pale katika Dimba la Taifa dhidi ya Simba Sports
Club ya Dar es salaam,Ikumbukwe katika mchezo
uliopita Timu ya Coastal Union waliichapa Bila
huruma Timu ya Simba Sports Club katika Uwanja
huo huo wa Taifa hivyo Kujizolea points zote tatu katika
mchezo huo...Timu ya Mgambo ilimaliza rasmi mazoezi
ya Kujiandaa na Ligi jana na Wanasema kila kitu kiko
sawa na Wanawaahidi washabiki wao kuwa mwaka
huu hawatawaangusha kama miaka minginne ambayo
inaonekana wanaponea Tundu ya Sindano kushuka
daraja.Kila la Kheri Mgambo Shooting,Kila la kheri
Coastal Union..Tanga kwanza.
No comments:
Post a Comment