Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Monday, September 15, 2014

Hili la Kocha Bora Lifanyiwe Kazi Isiwe Mazoea

Hapa nikiwa na ndugu Juma Mwambusi Kocha wa Mbeya City
Asalaam Aleikun Wapenzi wa Mgosi wa Sui Sports ZoneLigi kuu ya Soka Tanzania Bara Inapiga Hodi Kuanza Mwishoni mwa wiki hii katika Viwanja Mbalimbali vyaSoka Nchini Tanzania.
Hapa Kwetu Tanga Tunatarajia Mchezo Mkali kati ya Mgambo Shooting na Kagera Sugar timu ambayo Binafsi yangu inanisisimua sana kwa soka lakela kiumakini zaidi ni kama vile walivyo Mtibwa labda kwa Sababu wote ni wakata miwa.
Maoni yangu kwa TFF Ni
kuhusiana na Tuzo Binafsi za wanamichezo wahusika wa
ligi hiyo,Kuna Tuzo kadhaa hutolewa kama vile Mchezaji Bora
Kipa Bora,Mfungaji Bora,Refa Bora na Timu Bora pamoja
na Bingwa ambaye wala haina shida katika mchakato wa
kupatikana kwake kwani hapigiwi kura huyu...
Kocha Bakari Shime akifanya mahojiano naVyombo vya Habari
Ila leo mada yangu itahusu sana Tuzo ya Kocha bora ambayo mwaka jana ilitolewa kwa Juma Mwambusi
kocha wa Mbeya City ya Mkoani Mbeya,Hongera
kwake,Ila wadau wengi tunashindwa kuelewa amakuwekewa wazi Vigezo vya kupatikana kwa Kocha
bora,nina maana hapa..kama tatizo ni kwa timu,kushika nafasi ya juu kwa nini kocha bora asiwe wa Azam FC?Aje kuchaguliwa kocha huyu ambaye nafasi yake ilikuwa ya chini kuliko huyo?ina maana kuna zaidi ya hilo ili kuwa kocha bora sio lazimauwe bingwa,

                     Mgambo Ikiwa Mazoezi baada ya kuchukuliwa na Shime

Msimu uliopita tuliona maajabu ya Soka kwa timu iliyokuwa kama Imeshashuka daraja kubakizwadaraja,Mgambo Shooting Club ya Kabuku Handeni Tanga,Mpaka kufikia Raundi ya 14 Timu ilikuwa nafasi ya Mwisho kwa kuwa na Points 6 juu yake alikuwapo Ashanti united na Point zake 11,Kocha
wa Mgambo alichukua maamuzi magumu ya kuacha timu kwa kile alichokiita matatizo ya kifamilia japo kuna wakati alisikika akisema timu haifundishiki, Mikoba akapewa Bakari nyundo Shime anayetokea
EAGLE SPORTS ACADEMY kuinusuru timu hiyo, binafsi yangu alinipitia nyumbani kuniaga na kuniambiakuna mambo mawili kuwa Shujaa ama kuaibika ila nitakuwa shujaa tu..nikamuaga akaondoka kuelekea  Dar-es-salaam kuungana na timu na mechi ya raundi ya 15 Mgambo ilikutana na Ashanti United na Kuifunga magoli 2 kwa Bila pale katika uwanja wa Chamanzi
Azam Complex.
Bakari Shime Kazini
Kutokea hapo Mgambo haikurudi Nyuma  ilishinda mechi moja baada ya nyengine ikiwamo  kuwafunga watani wa jadi yanga na simba katika safari yake ya kujinusuru kushuka daraja na kutokea kujikusanyia points 5 kwa raundi ya kwanza ilijikusanyia point 20 raundi ya pili wakati huo Mbeya City walijikusanyia points 21 ambao hao walitoa kocha bora na kumbuka Bakari Shime alichukua timu na kucheza michezo pungufu round ya pili na bado aliinusuru timu kushuka daraja, Kumbuka Kocha huyu timu hakusajili yeye ameikuta tena iko hoi akafanya miujiza kama hiyo iweje asizingatiwe katika nafasi ya Ukocha Bora?ama kuna cha zaidi Mtuambie,Lakini huu si Muda wa kulaumiana kwa sasa ila kwa Maoni yangu Mimi kama mimi kama zilivyo Tunzo ya Mchezaji Bora na hii ya kocha bora nayo iwe na Michakato kama iyo,Narejea tuzo ya chezaji Bora inaanza na tuzo ya mchezaji Bora wa mechi,mwezi kisha inaangaliwa nani kapata nyingi ndio awe Mchezaji bora wa Msimu, na Kama mchakato ungeenda hivi kwa miezi yote ya kuendea mwishoni mwa ligi hakukuwa na kocha Bora zaidi ya Huyu wa Mgambo,Bakari Nyundo Shime Tukisoma kwa wenzetu kila mwezi kuna tuzo ya kocha bora basi na hapa kwetu iwepo ili kuondoa mazingira tata na ukakasi kwa Wadau wa Mpira na Makocha wenyewe pia kuondoa zigo la lawama pale TFF.
Yote kwa yote nampongeza Juma Mwambusi kwa Tuzo
Asalaaaaam






No comments:

Post a Comment