Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Monday, September 21, 2015

Wagosi wa Kaya Wafungua kwa Point Moja

Timu ya soka ya Coastal Union ya Tanga almaarufu
Wagosi wa Kaya jana walishindwa kuutumia vema
uwanja wao wa Nyumbani Mkwakwani katika mechi
ya vuta nikuvute wa Ligi kuu ya soka Tanzania bara
baina yao na TOTO Africans ya mwanza.Katika
mchezo huo ulioshuhudiwa na mashabiki wengi wa
kizungu ulikuwa mkali na mashambulizi ya kushtukiza
kwa kila Upande.Timu hiyo ya Coastal union ilipata
vichapo katika mechi mbili zilizopita kati yao na Yanga
na Ndanda F.C ,Ligi hiyo itaendelea tena katika uwanja
wa Mkwakwani kwa Mechi kati ya Coastal Union na
 Mwadui ya Shinyanga inayonolewa na Jamhuri Kihwelo
(JULIO)Aliyewahi kuionoa Coastal Union msimu uliopita.
na Jumapili kutakuwa na Mchezo kati ya African Sports
na NDANDA F.C Ya mtwara.

No comments:

Post a Comment