Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Tuesday, January 6, 2015

Mechi Nane Kuhitimisha Safari ya Matumaini ya Wana Kimanumanu..

Safari iliyobatizwa jina ya Matumaini ya African Sports
bado inaendelea Vyema kabisa ingawa sehemu iliyobaki
inahitaji Umoja,Mshikamano na Jitihada binafsi,Kila mdau
wa Tanga anahitajika kufanya sehemu yake.Safari hiyo ni
ngumu na ilishuhudia mechi tatu za mwisho nje ya Tanga
wana Kimanumanu wakikipiga na African Lyon ya Dar na
kupata Point tatu halafu wakasafiri mpaka Iringa kupambana
na LIPULI ya huko Shukrani kwa Goli la Kujifunga la wana
Kimanu manu likawapa Points tatu Lipuli,kisha wana Kimanu
wakarejea Dar tena kwa basi lao la Ratco walilopewa na
kampuni ya Ratco kwa ajili ya kusafiria tu wakakutana na Police
Dar na kupata ushindi mwembamba tena wa bao moja kwa Bila,
kwa maana hiyo mechi zao za Nje wamefanikiwa kupata alama
siita kati ya tisa hali inayoonyesha bado sio mbaya sana.
Msimamo wa ligi hiyo unaonyesha kuwa Majimaji ya Songea
wanaongoza kwa kuwa na Points 28 wakifuatiwa na LIPULI
NA AFRICAN SPORTS zenye alama 26 lakini LIPULI wanazidi
kwa tofauti ya Goli moja tu.Michezo iliyobaki kwa African Sports
wana Kimanu manu ni kama Ifuaatavyo
12-01-2015 Nyumbani na ASHANTI UNITED
15-01-2015 Nyumbani na TESEMA(KMC)
18-01-2015 Ugenini na VILLA SQUAD
22-01-2015 Nyumbani na KIMONDO FC
25-01-2015 Nyumbani na MAJIMAJI
28-01-2015 Nyumbani na JKT MLALE
01-02-2015 Ugenini na KURUGENZI FC
04-02-2015 Ugenini na FRIENDS RANGERS.
Kwa maana hiyo kuna mechi nane zilizobaki,tano mkwakwani na tatu nje.
Tunawatakia kila la kheri wana Kimanu manu.

No comments:

Post a Comment