Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Wednesday, December 31, 2014

Zimebaki Siku 20 tu kwa African Sports wana Kimanu manu Kukielewesha

Kikosi cha African Sports

Kikosi cha African Sports

Logo ya African Sports
Timu ya soka ya African Sports imeendelea vyema katika
mzunguko wa lala salama wa ligi daraja la kwanza tanzania
kwa kuwafunga African Lyon bao moja kwa Bila.Mchezo
huo ulikuwa wa vuta nikuvute ulichezwa uwanja wa Karume
Dar.African Sports ilijipatia Bao hilo kupitia kwa Mchezaji
wake Ali Kagawa.Timu hiyo ya African Sports kwa matokeo
hayo inakwea hadi nafasi ya pili kwa tofauti tu ya magoli dhidi
ya LIPULI ya Iringa watakayomenyana nayo leo hii kule mjini
Iringa.Ligi hiyo katika kundi la African sports Majimaji ya Songea
ndio wanaoongoza ligi na wanatarajiwa Kupambana na timu
ya KMC Ya kinondoni katika uwanja wa Mkwakwani mjini
Tanga.Kila la Kheri African Sports wana Kimanu manu.

No comments:

Post a Comment