Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Tuesday, December 30, 2014

Inabidi Wanaojirusha Wafungiwe...Wenger

Arsenal Wenger
Kocha mkuu wa Arsenal,Arsene Wenger ametabainisha
kuwa Chama cha Mpira nchini England kiweke utaratibu
wa kuunda kamati ya watu watakaoshuhulika na wachezaji
wanaojirusha kwa kumdanganya Refa uwanjani.Wenger
alikiri kuwahi kuwa na Wachezaji wanaojirusha Uwanjani
kwenye timu yake japo analipinga vikali swala hilo na ni
juu ya Wachezaji wenyewe kujirusha ama kutojirusha.Wenger
amesema kuwa njia pekee ni kuwafungia wale ambao Refa
hakuwaona wakati mchezo ukiendelea ili kuwashikisha adabu.
"Lazima tuwaadhibu wanajirusha baada ya mechi,ila tatizo
litakuwa je walifanya kusudi ama walifanya kwa bahati mbaya"
Njia pekee ya wachezaji kuachana na tabia hii ni wao kujua
kwamba wakifanya watakumbana na adhabu kali.Kocha wa
Chelsea Jose Mourinho amebaini Kampeni dhidi ya timu yake
baada ya makocha wengi kushutumu wachezaji wake katika
swala hilo la kujirusha,na hiyo ni kabla ya tukio la
Cesc Fabregas katika mechi ya Draw dhidi ya Southampton
ambapo alipewa kadi ya njano kwa kujirusha.Wenger alisema
ni jambo la kawaida kwa kila Klabu,Tuliwahi kuwa na Eduardo
pamoja na Roberto Pires,wa kulaumiwa ni wachezaji tu sio
Vilabu.Unatakiwa kuchaguwa kuwa mkweli ama Muongo na ni
ufumbuzi mgumu kwa wachezaji na Kinachohitajika ni kwa
wachezaji kuwa wa kweli.Wakati wachezaji wakianza kujirusha
ama wakijirusha ni vigumu kwa Refa kuwabaini,Hata ikitokea
umeongea na wachezaji wenye hulka hiyo wakiingia mchezoni
watafanya tena..alimalizia Wenger.

No comments:

Post a Comment