Timu ya soka ya Coastal Union almaarufu Wagosi wa kaya
leo walikuwa Mbeya wakipepetana na Timu ya Prisons ya
huko katika mchezo mkali na wa kusisimua.Mchezo huo
umechezwa katika uwanja uliojaa Maji kutokana na Mvua
kubwa iliyonyesha Jijini Mbeya.Coastal wanapaswa kujilaumu
wenyewe baada ya kukosa mabao mengi pamoja na kutawala
mchezo huo.Kesho timu nyengine kutoka Tanga Mgambo JKT
Itajitupa uwanjani kupambana na Polisi Moro.
No comments:
Post a Comment