![]() |
| Rodgers akiwapa maelekezo wachezaji wake |
![]() |
| Luis Van Gaal akiongea na Msaidizi wake Ryan Giggs |
Van Gaal amesema kuwa makelele yanayopigwa na makocha
wenzake wa English premier League hayana umuhimu wowote
kwa wachezaji kwani hawaelewi wala kufuata wanachoambiwa
na makocha hao.Makelele ya mashabiki uwanjani yanazidi kelele
za makocha wanazopiga makocha kwa wachezaji wao hivyo
kuwa haina maana kwa kocha kusimama pembeni ya kiwanja na
kuanza kupiga mayowe.Kocha huyo ambaye hajawahi kuonekana
hata siku moja akisismama pembeni ya kiwanja akipiga kelele kwa
wachezaji wake amesema huwa anampa maelezo Ryan Giggs kocha
wake msaididzi kama ikibidi lakini sio yeye kusimama.Tunawafunza
wachezaji wiki nzima kusoma mchezo na kubadilika kutokana na
mazingira hivyo haina umuhimu kwetu kusimama simama kila mara
kutoa maelezo.


No comments:
Post a Comment