Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Wednesday, December 3, 2014

Manchester United Mwendo mdundo

Juan Matta akifanya yake Dimbani
 Timu ya soka ya Manchester United Almaarufu Mashetani wekundu
Jana walijipatia ushindi wao wa Nne mfululizo kwenye ligi kuu ya soka
Nchini England kwa kuwabamiza timu ya Stoke city kwa mabao 2-1.
Mchezo huo uliochezwa kwenye Dimba la Old trafford ulishuhudia kwa
mara Nyengine tena kiwango bora kabisa cha Kiungo wake aliyeanza
kwa kusuasua katika timu hiyo msimu uliopita Maroune Felaini,Kiungo
huyo kutoka Everton awali katika siku za mwanzo za maisha yake Old
Trafford alihusishwa na kuuzwa tena kwani alionyesha kiwango cha Chini
sana chini ya kocha David Moyes aliyetimuliwa mwishoni mwa msimu
uliopita na nafasi yake kuchukuliwa kwa Muda na Ryan Giggs Kisha
baadae akaja Luis Van Gaal huku Giggs akiwa msaidizi wake,Man united
walianza kwa kulisakama lango la Stoke City na Kiungo wake Ander
Hereira alikosa bao la wazi kabisa katika mchezo huo kabla ya Fellaini
hajaruka kichwa safi na kufunga goli la kwanza kwa Man United,Stoke
walipeleka mashambulizi na kufanikiwa kufunga Goli kupitia kwa steven
zonzi,Hadi mapumziko stoke 1-man 1,kipindi cha pili kilianza kwa timu
zote kutafuta ushindi lakini ilikuwa ni manchester united tena kupitia Juan
mata kufuga goli la pili na la ushindi kwa mashetani hao wekundu,kwa
ushindi huo man united wanafikisha alama 25 huku wakiendelea kushika
nafasi ya nne alama moja nyuma ya Southampton wanaominyana na Arsenal
leo,
Maroune Fellaini akishangilia Bao

No comments:

Post a Comment