Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Friday, November 14, 2014

Wachezaji wa Mgambo shooting ya Tanga wageuka LULU

Malimi Busungu
 Wachezaji wa timu ya soka ya Mgambo shooting ya Tanga wamegeuka Lulu baada ya kufanya vyema katika Mzunguko wa kwanza wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara VODACOM timu hiyo ya Mgambo shooting ambayo miaka ya Nyuma ilikuwa timu ya Kawaida tu inayopigania kutoshuka daraja katika ligi Imegeuka kuwa mwiba kwa sasa kwa timu zote zinazoshiriki ligi hiyo,Mabadiliko hayo yametokana na kubadilisha Benchi la Ufundi la timu hiyo kutokana na kujiuzulu kwa aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Mohamed Kampira,Mikoba akapewa Bakari Nyundo Shime ambaye aliikuta timu hiyo ikiwa na Points 6 na ikiwa mkiani mwa ligi hiyo
Malimi Busungu
 Bakari Shime alipambana na kuinusuru timu hiyo kubaki daraja kwa kujizolea alama 20 zaidi,Msimu huu timu hiyo ilianza ligi vyema na kuwafanya Vigogo wa soka kuitazama kwa jicho la pili,Mechi ya mwisho kati yake na Yanga kabla ligi kusimama ndipo Timu mbalimbali zilipoanza kutuma maombi ya kuwachukua Nyota wake kadhaa baada ya kuonyesha Kandanda safi na la kuvutia Uwanja mkubwa wa Taifa dhidi ya Yanga,Nyota anayeongozwa kwa kuuliziwa kwa mujibu wa Viongozi wa Mgambo ni Malimi Busungu ambaye aliibuka kuwa Nyota wa mchezo katika mechi ya Yanga na Kumfanya kocha Mkuu wa Timu hiyo
Bakari Shime
 Marcio Maximo kuwaomba Viongozi wake wajitahidi kwa hali na mali mchezaji huyo akipigie katika kilabu hicho cha Jangwani,Malimu Busungu kwa Mujibu wa Uongozi wa timu sio Askari wa Jeshi kama walivyo wachezaji wengine,Mgambo shooting kwa sasa wako mapumziko mpaka tarehe 26 mwezi huu kwa ajili ya kujiandaa na Mzunguko wa Pili,Kila la kheri Mgambo Shooting.
Mgambo shooting wakishangilia Bao

Malimi Busungu akijiandaa kupiga Penalt

Kikosi cha Mgambo Shooting

No comments:

Post a Comment