Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Thursday, November 13, 2014

Safari ya Matumaini Ya wana Kimanumanu Imefufuka


Chambega akijiandaa Kuingia
 Timu ya soka ya African sports ya Tanga jana Ilifufua matumaini yake ya kuelekea Ligi kuu Tanzania Bara mwakani kwa kutoka kimasomaso  ugenini kwa kuwafunga JKT Mlale mabao mawili kwa moja,,magoli hayo yalifungwa na Ramadhani Hamidu(mwanzo Mgumu) na Hassan Gurudumu mshambuliaji hatari wa African Sports  mwenye kuongoza kwa kufunga mpaka sasa,
Kikosi cha African Sports

Striker Hatari wa Eagle Herbert Ukindo

Captain wa Eagle.Van Toba
 Timu hiyo ya African Sports awali ilikuwa imepoteza michezo miwili ugenini mjini Mbeya na Songea dhidi ya majimaji ya Songea,African sports ya Tanga baada ya ziara ya Nje ya Mkoa wa Tanga inatarajiwa kurejea kusubiria mchezo dhidi ya Ashanti United,Kwingineko katika ligi daraja la Tatu ngazi ya Mkoa Timu ya Eagle Academy juzi iliwapa kipigo cha Mbwa Mwizi timu ya Gurudumu ya mjini hapa,Nyota ya mchezo huo alkua mshambuliaji wao hatari Herbert Lukindo kwa Kupachika wavuni mabao mawili na kumfanya kuwa moja ya washambuliaji wanaoongoza kwa magoli mpaka sasa.
Eagle academy katika Mishe mishe

No comments:

Post a Comment