BRENDAN RODGERS ASEMA AMEKALIA KUTI KAVU LIVERPOOL
KOCHA
Brendan Rodgers amekiri kwamba amekalia kuti kavu baada ya Liverpool
kuchapwa mabao 3-1 na Crystal Palace jana na sasa anapambana kuokoa
kibarua chake.
Rodgers
amesema alikuwa na mazungumzo na wamiliki wa Liverpool ambao ni
Wamarekani juu ya mwenendo mbovu wa timu hiyo, ambao unawafanya wazidiwe
pointi 18 na vinara Ligi Kuu ya England, Chelsea.
Brendan Rodgers yuko katika wakati mgumu Liverpool akiwa ameshinda mechi mbili tu katika Ligi tangu Agosti
No comments:
Post a Comment